• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshambuliaji wa Kanisa la Texas atambuliwa kuwa ni askari wa zamani wa jeshi la anga

    (GMT+08:00) 2017-11-06 19:27:55

    Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa mshukiwa wa mauaji katika kanisa la Texas awali alitumikia jeshi la anga la nchi hiyo na ameondoshwa jeshini na kushushwa cheo kwa madai ya kumshambulia mkewe na mwanawe.

    Msemaji wa jeshi la anga Ann Stefanek amesema Devin Kelly alifungwa kwa miezi 12 baada ya kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi. Mshukiwa huyo akiwa amevalia nguo nyeusi amewafyatulia risasi watu 26 ndani ya na nje ya kanisa la Sutherland Springs, umbali wa km 300 kutoka Huston magharibui, Texas na baadaye kuondoka. Hivi sasa uchunguzi unaendelea kwa msaada wa polisi, FBI na idara nyingine. Kwa sasa takriban watu wanane wamejeruhiwa na wanatibiwa hospitalini.

    Wakati huohuo rais wa Marekani Donald Trump ambaye yuko ziarani nchini Japan, amelaani vikali tukio hilo na kuahidi uongozi wake utasaidia uchunguzi wa shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako