• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali:Watumishi wana sababu ya kutabasamu mwezi huu

    (GMT+08:00) 2017-11-06 20:22:30

    Watumishi wa umma nchini Tanzania mwez huu watapewa nyongeza ya mwaka ya mishahara yao, Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi amesema hayo.

    Akizungumza na viombo vya habari, Dk Abbasi amesema nyongeza hiyo itaonekana kwenye mishahara ya watumishi wa Umma kuanzi mwezi huu.

    Aidha amesema baada ya serikali kushughulikia wafanyakazi hewa, imeweza kuokoa Sh bn 238 na wafanyakazi wenye vyeti 'feki' Sh bn142.

    Jumla ya Sh bn 380 imeweza kuokolewa.

    Hata hivyo, msemaji huyo ameeleza kuwa fedha ambazo zimepatikana baada ya kudhibiti ubadhirifu na kuongezeka kwa mapato serikali hadi kufikia Sh14trn kwa mwaka yameiwezesha serikali kutoa elimu bure, kuboresha huduma za afya pamoja na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya usafirishaji na maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako