• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Japan na Marekani waamua kutatua suala la kutokuwa na uwiano wa biashara kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-11-07 09:05:39

    Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe na rais Donald Trump wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Japan wamefanya mazungumzo mjini Tokyo, na kukubaliana kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao, na kuamua kutatua suala la kutokuwepo kwa uwiano wa biashara ndani ya mfumo wa mazungumzo ya kiuchumi.

    Hii ni mara ya kwanza kwa rais Trump kufanya ziara nchini Japan tangu ashike madaraka ya urais. Rais Trump amesema ni lazima kubadilisha hali ya kutokuwa na uwiano wa biashara, na kupunguza urari mbaya wa biashara ya Marekani kwa Japan. Amesisitiza Marekani inatumai kuboresha uhusiano wa kiuchumi na Japan, na kujenga uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa haki, huru na wa kunufaishana.

    Bw. Shinzo Abe amesema Japan na Marekani zimekubaliana kufanya mazungumzo ya kina ndani ya mfumo wa mazungumzo ya kiuchumi, na kujadili kutatua suala la kutokuwepo kwa uwiano wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako