• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Marekani nchini China asema mkutano wa Rais Xi Jinping na Rais Trump utakuwa wa kihistoria

    (GMT+08:00) 2017-11-07 09:20:03

    Balozi wa Marekani nchini China Bw Terry Branstad amesema mkutano unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni kati ya Rais Xi Jinping wa China na Rais Donald Trump wa Marekani utakuwa muhimu na wa kihistoria.

    Balozi Branstad amesema Rais Xi na Rais Trump wanaelewana vizuri, na kama wataondoa tofauti zilizopo, kazi zilizopo zitafanyika kwa urahisi.

    Amesema anatarajia kuwa kwenye ziara ya Rais Trump itakayoanza kesho hapa Beijing, pande mbili zinaweza kutatua maswala magumu.

    Balozi huyo pia amesema ajenda kuu kwenye mazungumzo kati yao zitakuwa ni suala la nyuklia la peninsula ya Korea na biashara kati ya pande mbili. Rais Trump anatarajia kuja na ujumbe wa wafanyabiashara wanaotarajia kusaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa uzalishaji viwanda na nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako