• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ombi la kupinga tena ushindi wa rais Kenyatta lawasilishwa kwenye mahakama kuu ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-07 09:21:21

    Mwanasiasa wa Kenya Bw. Harun Mwau amewasilisha ombi la kupinga tena ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu mpya uliofanyika tarehe 26 Oktoba kwenye mahakama kuu ya Kenya. Ombi hilo linatarajia kuahirisha kuapishwa kwa rais Kenyatta wakati mahakama hiyo inapitia ombi hilo.

    Katika ombi hilo Bw. Mwau amelaani kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ilikiuka sheria kwa kushindwa kuwapitisha wagombea wanane kwenye mchujo kwa mujibu wa sheria na maagizo ya mahakama kuu.

    Pia amedai kuwa tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake Bw. Wafula Chebukati walishindwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia rahisi na wazi, kwa kuwa wagombea hawakupatikana kwa njia halali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako