Tume ya ngazi ya juu ya Uchaguzi ya Libya imeamua kusaini makubaliano kuhusu utoaji wa msaada wa ufundi na vifaa na Umoja wa Mataifa, ili kuunga mkono uchaguzi wa rais na wabunge utakaofanyika mwaka kesho nchini humo.
Mkuu wa tume hiyo Bw. Imad Al-Sayah amesema kuwa tume hiyo inasubiri Ujumbe wa utoaji wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kukamilisha uratibu kati ya Libya na nchi zinazotoa msaada, kwa kuunga mkono uchaguzi utakaofanyika nchini humo.
Pia amesisitiza kuwa Libya iko tayari kufanya uchaguzi ndani ya miezi minne tangu bunge la nchi hiyo lilipopitisha sheria ya uchaguzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |