Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi makamu wake Bw Emmerson Mnangagwa kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu. Akitangaza uamuzi wa Rais Mugabe, waziri wa habari wa nchi hiyo, Bw Simon Moyo, amesema katiba ya Zimbabwe inampa Rais madaraka ya kufanya hivyo. Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitano kwa Rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake, baada ya kufanya hivyo mwaka 2014 alipomfukuza Bibi Joyce Mujuru kwa madai ya kula njama za kumpindua.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |