• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahudhuria mkutano wa 7 wa nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ufisadi

    (GMT+08:00) 2017-11-07 17:54:09

    Mkutano wa 7 wa nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ufisadi umefunguliwa jana huko Vienna nchini Austria. Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qian Hongshan ameongoza ujumbe wa China na kuhudhuria mkutano huo.

    Bw. Qian amesema kwenye mkutano huo kuwa China inatilia maanani sana kazi ya kupambana na ufisadi, na inakamilisha sheria na utaratibu kuhusu kupambana na ufisadi bila kusita, kuimarisha usimamizi kwa matumizi ya madaraka na kufanya ushirikiano wa kimataifa kuhusu kupambana ufisadi. Vilevile ameeleza uamuzi muhimu wa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi, ukisisitiza kuhimiza utungaji wa sheria ya kitaifa ya kupambana na ufisadi, kuzidisha mageuzi kuhusu utaratibu wa usimamizi wa taifa na kutimiza lengo la kusimamia watumishi wote wa serikali hatua kwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako