• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza msimamo wake kuhusu suala la polisi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-11-07 18:36:29
    China imetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kufikiria kwa makini changamoto, majukumu na maendeleo ya baadaye kuhusu kazi za polisi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
    Hayo yamesemwa na kaimu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao jana wakati wa mjadala wa wazi uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu suala la polisi wa kulinda amani wa Umoja huo. Balozi Wu amesisitiza umuhimu wa kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni za kimsingi za kulinda amani, na kazi zinazofanywa na polisi hao zinapaswa kuwa wazi, kutekelezeka, kulingana na hali halisi ya nchi wanazopelekewa polisi na kuweka wazi vipaumbele. Pia amesema sekretariti ya Umoja wa Mataifa inapaswa kutoa uungaji mkono wenye ufanisi kwa polisi kutekeleza majukumu yao, na nafasi zinazotolewa na nchi zinazotuma polisi zinapaswa kutiliwa maani.
    Tangu itume kwa mara ya kwanza polisi wa kulinda amani kwa Umoja wa Mataifa mwaka 2000, China imetuma askari zaidi ya 2,600 kwa maeneo ya majukumu ya kulinda amani. Kwa sasa, polisi wa kulinda amani wa China zaidi ya 150 wanatekelezaji majukumu yao nchini Sudan Kusini, Cyprus na Afghanistan.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako