• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wa Uganda waanza mgomo wa nchi nzima kupinga mishahara midogo

    (GMT+08:00) 2017-11-07 18:42:16

    Madaktari wa Uganda wameanza mgomo wa nchi nzima kufuatia serikali kushindwa kujibu matakwa yao kuhusu nyongeza ya mshahara na kuboresha mazingira ya kazi katika hospitali za umma.

    Madaktari hao wanaoongozwa na Shirikisho la Matibabu la Uganda UMA wameanza mgomo baada ya kukataa wito wa kusimamisha hatua uliotolewa na waziri mkuu Bw. Ruhakana Rugunda, na maofisa wa wizara ya afya katika mkutano wa pande mbili uliofanyika jana huko Kampala.

    Mwenyekiti wa UMA Bw. Ekwaro Obuk amesema, mgomo huo utaendelea hadi serikali itakapokidhi mahitaji yao kuhusu kuboresha malipo, upungufu wa dawa na vifaa ili waweze kufanya kazi vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako