• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri Ummy wa afya asema hakuna upungufu wa dawa Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-11-07 19:25:22

    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania Ummy Mwalimu amesema hakuna tatizo la dawa nchini kwani serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha kuwa zinapatikana muda wowote.

    Alitoa majibu hayo wakati akimjibu mbunge wa Siha katika kipindi cha Maswali na Majibu cha Bunge la Tisa mjini Dodoma, Dk Godwin Mollel aliyetaka kujua hatua inayochukua serikali kukabiliana na upungufu wa dawa.

    Waziri Ummy alisema kuwa wilaya zote, ikiwemo Siha, kuna dawa dawa zote 135 muhimu na kumtaka kuachana na taarifa zilizopitwa na wakati. Hata hivyo, Ummy ameongeza kuwa kati ya dawa zinazoagizwa, ni asilimia chini ya tano tu zinazoharibika, jambo ambalo linaendana na viwango vya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako