• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yasema wapiganaji wa kundi la Boko Haram wapata hasara kubwa

    (GMT+08:00) 2017-11-08 09:55:14

    Mwenyekiti wa serikali ya eneo la Madagali la Nigeria Bw Yusuf Mohammed jana amesema wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamepata hasara kubwa walipojaribu kuvamia mji wa Gulak, ulioko katika jimbo la Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

    Wapiganaji hao walipambana na jeshi la serikali kwa muda wa saa kadhaa walipojaribu kuingia katika mji huo usiku wa jumatatu.

    Bw. Yusuf amesema wapiganaji wa Boko Haram walipata hasara kubwa, lakini idadi halisi ya waliouawa bado haijathibitiwa. Lakini ametangaza kuwa wanawake wawili, mmoja mwenye umri wa miaka 70 na mwingine mwenye umri wa miaka 30, walipigwa risasi walipojaribu kukimbia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako