• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Assad wa Syria azungumzia ushindi wa majeshi ya Serikali

    (GMT+08:00) 2017-11-08 10:05:44

    Rais Bashar Al Assad wa Syria amesema ushindi wa majeshi ya serikali yake dhidi ya makundi ya kigaidi yameisaidia Syria kujiepusha na mpasuko.

    Rais Assad amesema hayo kwenye mazungumzo yake na Ali Akbar Velayati ambaye ni mshauri mkuu wa kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

    Amesisitiza kuwa vita vinavyoendeshwa na majeshi ya serikali si kwa ajili ya kuyaangamiza makundi ya kigaidi tu, bali pia ni vita ya kuzuia njama za kuyatumia makundi hayo kuigawa Syria.

    Wawili hao pia wameafikiana na dhana kuwa vikwazo vingi kutoka kwa jumuiya mbalimbali za kimataifa dhidi ya Iran vinatokana na ushindi huo dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako