China na Marekani zimehimizwa kuanzisha uhusiano mpya kati ya nchi kubwa ili kunufaisha dunia nzima.
Mchambuzi wa chuo Kikuu cha Bogazic cha Uturuki Bw. Kadir Temiz amesema, China na Marekani ni nchi muhimu ambazo zinaweza kuathiri kwa kiasi kubwa utulivu wa siasa na uchumi wa dunia. Jambo lolote linaloharibu umuhimu huo linaweza kusababisha msukosuko wa uchumi wa dunia na utaratibu wa kisiasa.
Amesema anatarajiwa kuwa ziara ya rais Donald Trump nchini China itatoa fursa mpya, licha ya kuwepo kwa tofauti kati ya China na Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |