• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande zinazopambana Yemen kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-11-08 18:46:15

    China imetoa mwito kwa pande zinazopambana nchini Yemen kufikia ufumbuzi unaoridhisha pande zote haraka iwezekanavyo kwa njia ya mazungumzo, ili kurejesha utulivu na hali ya kawaida nchini Yemen.

    Hivi karibuni, Saudi Arabia ilifanikiwa kuzuia kombora lililorushwa na kundi la Houthi dhidi ya uwanja wa ndege wa Riyadh, na kuishutumu Iran kuwa inatoa uungaji mkono wa kisilaha kwa kundi la Houthi.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amezungumzia hali ya hivi sasa ya sehemu hiyo akisema, mapigano yaliyodumu kwa miaka miwili na nusu nchini Yemen, yameleta athari mbaya kwa usalama na utulivu wa kanda hiyo. Kipaumbele ni kuzihimiza pande mbalimbali kufikia makubaliano kwenye msingi wa maazimio husika ya jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako