• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti za Kenya zakosa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato

    (GMT+08:00) 2017-11-08 19:44:51

    Kaunti 45 nchini Kenya zilikosa kufikia malengo ya ukusanyaji ushuru katika mwaka uliopita wa kifedha.

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi wa Bajeti nchini Kenya.

    Ni kaunti mbili pekee ambazo zilifikia malengo ya kukusanya mapato.

    Ripoti ya Mkaguzi wa Bajeti inasema kuwa kaunti ya Marsabit ilikusanya asilimia 107.3 huku kaunti ya Turkana ikifikisha asilimia 103.5 ya makadirio yao.

    Kwenye ripoti hiyo, inayoangazia jinsi kaunti mbalimbali zilivyotumia fedha zake, Mkaguzi wa Fedha Bi Agnes Odhiambo alisema kwamba ni Sh32.52 bilioni zilikusanywa kati ya Sh57.66 bilioni zilizokusudiwa.

    Aidha, Marsabit ilikusanya Sh128.7 milioni kati ya Sh120 milioni zilizokusudiwa, huku Turkana ikikusanya Sh186.3 milioni kati ya Sh180 milioni zilizokusudiwa.

    Kwenye mpango huo, Kaunti ya Nairobi ilikusanya Sh10.9 bilioni, ikifuatwa na Mombasa na Kiambu, zilizokusanya Sh3.17 bilioni na Sh2.03 bilioni mtawalia.

    Kaunti zilizokusanya kiwango kidogo zaidi cha fedha ni Wajir, Mandera na Tana River, zilizokusanya Sh75.9 milioni, Sh55.8 milioni na Sh27.4 milioni mtawalia.

    Kaunti za Busia, Garissa, Isiolo, Kajiado, Kakamega, Kilifi, Kirinyaga,Kisii, Kitui na Machakos hazikufikisha asilimia 50 ya malengo yake. Zingine ni Mandera, Nyamira, Taita-Taveta, Tana River, Tharaka-Nithi, Trans Nzoia, Vihiga na Wajir.

    Fedha hizo hukusanywa kutoka kwa kodi za burudani, biashara, ada za magari ya umma, zile za uegeshaji ,miongoni mwa nyenginezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako