• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bajeti ya 2018/2019 Tanzania inatarajiwa kuwa Sh.trilioni 32.476.

  (GMT+08:00) 2017-11-08 19:45:12

  Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania Dk Philip Mpango amesema bajeti ya tatu ya serikali ya awamu ya tano inatarajiwa kuwa Sh.trilioni 32.476.

  Waziri Mpango aliyasema hayo wakati alipokuwa akiwasilisha bungeni jana mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa mwaka 2018/2019 na Mwongozo wa Maandalizi ya Bajeti ya mwaka ujao wa kifedha .

  Anasema maoteo ya wali yanaonyesha kiwango hicho cha fedha kinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hicho ikiwa ni ongezeko la Sh.bilioni 764 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka huu ya Sh.tril 31.712.

  Dk.Mpango alisema maoteo ya Sh.trilioni 32.476 kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha yatathibitishwa baada ya kufanya uchambuzi wa mwenendo wa utekelezaji wa bajeti katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017/2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako