• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaipatia Uganda msaada wa $30m (Shs 109.3bn) kuboresha forodha

  (GMT+08:00) 2017-11-08 19:48:24

  Serikali ya China imekubali kusaidia mradi wa ujenzi wa forodha ya kisasa nchini Uganda kwa kutoa msaada wa $30m (Shs109.3b).

  Mkataba wa msaada huo ulitiwa saini mjini Beijing wiki iliyopita kati ya Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kasaija na Naibu Waziri wa Biashara wa Serikali ya watu wa China Dkt Qian Keming.

  Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Balozi wa Uganda nchini China Chrispus Kiyonga, Kamishna wa Mamalka ya Mapato kitengo cha Forodha nchini Uganda Dicksons Kateshumbwa na maafisa wengine wakuu wa serikali.

  Mkataba huo ulitiwa saini wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kamisheni ya pamoja ya biashara,uchumi,uwekezaji na ushirikiano wa kiufundi uliofanyika jijini Beijing.

  Msaada huo utaipiga jeki mamlaka ya mapato Uganda (URA) na kuweza kuwa na teknolojia na mifumo ya kisasa ya ukaguzi.

  Pia itasaidia katika huduma za forodha,uimarishaji wa miundomsingi ya mipakani ,miongoni mwa mambo mengine.

  Kwa upande wake Kasaija aliishukuru serikali ya China kwa msaada huo na kusema kuwa msaada huo utachangia kupunguza kupotea kwa mapato na pia kuimarisha biashara na usimamizi wa mipakani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako