• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bodi ya usimamizi wa manunuzi ya umma yatoa ruhusa ya ukarabati wa uwanja wa ndege wa Moi kwa ghrama ya Sh7b.

  (GMT+08:00) 2017-11-08 19:48:49

  Bodi ya uangalizi na usimamizi wa manunuzi ya umma (PPARB) nchini Kenya imetoa ruhusa ya uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Moi mjini Mombasa kwa gharama ya Sh7bn.

  Uboreshaji huo utajumuisha ukarabati wa mataa na kuongeza kiwango cha umeme na maji.

  Bodi hiyo ya ya uangalizi,ambayo inasimamiwa na wakili Paul Gicheru iliamua kuwa mamlaka ya viwnaja vya ndege nchini (KAA) ilifuata taratibu zote zinazohitajika wakati ilipopeana kandarasi kwa kampuni ya ufaransa ya Sogea Satom and Razel-Bec JV.

  Uboreshaji huo unalenga kuimarisha uwezo na ufanisi wa uwanja huo wa ndege,na unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) chini ya mradi wa usafiri wa Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako