• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya mashambulizi dhidi ya maeneo ya kidini nchini Afghanistan yaongezeka kwa kasi

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:16:09

    Tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan imesema idadi ya mashambulizi dhidi ya maeneo ya kidini na waumini inaendelea kuongezeka kwa kasi tangu mwezi januari mwaka jana.

    Ripoti imesema tangu mwanzo wa mwaka jana, mashambulizi 42 yametokea na kusababisha vifo vya watu 261 na wengine 572 kujeruhiwa. Idadi hiyo ni mara mbili ya idadi ya ujumla ya vifo vya watu katika mashambulizi kama hayo tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2015.

    Ripoti hiyo pia imetoa wito pande zinazopambana kufuata sheria husika, kusimamisha mashambulizi ya kimabavu dhidi ya waumini na kuchukua hatua zaidi kuhakikisha usalama wa jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako