• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Libya yaukomboa mji wa Warshaffana

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:38:42

    Jeshi la Libya limetangaza kuwa, kwa kushirikiana na vikosi vya umoja wa mataifa vimefanikiwa kuukomboa mji wa Warshaffana baada ya kuliangamiza jeshi linalopingana na serikali ya umoja inayoongoza Libya kwa sasa. Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa majeshi ya serikali ya ukanda wa magharibi wa nchi hiyo, Jenerali Osama Jweli, inaeleza kuwa viongozi wa jeshi la waasi wamekamatwa na wengine wakiripotiwa kukimbia.

    Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya umeeleza kusikitishwa na matukio ya mauaji dhidi ya raia wanaoishi maeneo ya karibu na mji wa Warshaffana, hivyo wamezitaka mamlaka kuhakikisha usalama wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako