• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Trilioni 4 zawekewa kwenye mbolea

  (GMT+08:00) 2017-11-09 20:05:37

  Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea nyaraka za maombi ya usajili wa kampuni za kuzalisha mbolea ambazo uwekezaji wake una thamani ya dola za Marekani bilioni 1.9 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh trilioni 4.

  Kampuni hizo ni Ferrostaal kutoka Ujerumani na Haldor Topsoe ya Denmark ambazo zimekuja kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea ya chumvi katika eneo la Kilwa Masoko mkoani Lindi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amesema mradi huo wa mbolea utatumia rasilimali ya gesi asilia inayopatikana hapa nchini katika shughuli zake za uzalishaji na utakuwa ukizalisha tani milioni 1.3 za mbolea kwa mwaka.

  Mbali na kiwango cha tani milioni 1.3 za mbolea zitakazokuwa zikizalishwa kila mwaka, mradi huo pia utaajiri Watanzania 4,500 na wageni 300.

  Mwambe alisema ukubwa wa mradi ni ujumbe tosha kwa wawekezaji mbalimbali duniani kwamba Tanzania ni mahali panapofaa kwa uwekezaji kwa kuwa kuna mazingira rafiki, serikali inayoaminika na kuwepo kwa mfumo unaosaidia kupata uwekezaji mwingi.

  Alisema uwekezaji huo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya viwanda lakini pia kwa kipindi kirefu kumekuwa na changamoto katika sekta ya kilimo kutokana na kiasi kikubwa cha mbolea kuagizwa kutoka nje, jambo ambalo kiuchumi halina afya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako