• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Rais Uhuru Kenyatta akataa kusaini mswada wa wakimbizi kumiliki biashara

  (GMT+08:00) 2017-11-09 20:06:58

  Rais Uhuru Kenyatta amekataa kusaini mswada wa kuwaruhusu kisheria wakimbizi kumiliki biashara ardhi na biashara pamoja na kilimo.

  Mswada huo wa wakimbizi ulilenga kuwanufaisha wakimbizi na kuwapa suluhu la kudumu la kuwapa uwezo wa kujitegemea badala ya kusubiri usaidizi wa wafadhili.

  Kisheria,wakimbizi wa Kenya hawaruhusiwi kufanya kazi.

  Rais Uhuru Kenyatta amependekeza mswada huo kuregeshwa bungeni na kujadiliwa upya kabla ya kutoa fursa ya wakenya kutoa maoni yao.

  Kipengee muhimu cha mswada huo kinapendekeza wakimbizi kupewa fursa ya kuajiriwa rasmi.

  Mswada huo uliwasilishwa na mbunge wa Ndhiwa Agostinho Neto mwezi juni mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako