• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya;Biashara ya mafuta ya Kenya yaahirishwa hadi mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2017-11-09 20:07:22

  Serikali ya Kenya imeahirisha kuanza kwa biashara ya mafuta kutoka Turkana iliopangwa kuuanza mwezi Disemba mwaka huu.

  Kampuni ya Tullow Oil inayosimamia mradi huo imetangaza kwamba Kenya itaanza kuuza mafuta yake mwaka ujao mwezi Januari.

  Wizara ya kawi nchini Kenya awali ilitarajia mauzo ya kwanza ya mafuta ya Kenya mwezi Juni mwaka huu kabla ya kuahirisha hadi Disemba na sasa paka mwaka ujao.

  Waziri wa kawi Charles Keter amesisitiza kwamba hitilafu na utata wa bomba kuu la mafuta la kusafirisha mafuta hayo kutoka Lokichar Turkana hadi Mombasa ni moja ya sababu ya kuchelewa kwa mauzo hayo.

  Aidha mafuriko ya mvua yaliosababishwa uharibifu wa daraja la Kainuk limechangia hatua hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako