• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha Simbas ya Kenya kitakachovaana na Chile chatajwa

  (GMT+08:00) 2017-11-10 09:15:37

  Kocha Jerome Paarwater jana alitaja kikosi cha Kenya kitakachovaana na Chile katika mechi ya ufunguzi ya shindano la raga la Cup of Nations litakalofanyika leo mjini Hong Kong. Katika mechi hii itakayopeperushwa moja kwa moja kupitia mtandao wake wa facebook wa Shirikisho la Raga la Hong Kong, raia huyu wa Afrika Kusini ameamua kufanya mabadiliko matatu katika kikosi kilichoanza mechi dhidi ya Dragons ya Hong Kong ambayo Simbas ya Kenya ilinyukwa 43-34 jijini Nairobi hapo Agosti 26, 2017. Vijana wa Paarwater hawajawahi kukutana na Chile. Mchuano huu unaweza kuenda upande wowote hasa kwasababu timu hizi pia zinakaribiana sana katika viwango bora vya raga duniani. Kenya inashikilia nafasi ya 27 kwa alama 56.21 nayo Chile ni nambari 27 kwa alama 54.76.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako