• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa APEC wahakikisha ahadi za kutimiza ongezeko endelevu na shirikishi

    (GMT+08:00) 2017-11-10 09:59:41

    Mkutano wa mawaziri wa APEC umepitisha nyaraka zitakazokabidhiwa kwa viongozi wa nchi za APEC, kuhusu kupunguza tofauti ya maendeleo na kuhimiza masikilizano ya uchumi, fedha na jamii.

    Naibu waziri mkuu wa Vietnam ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Pham Binh Minh amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, mkutano huo umesisitiza umuhimu wa mageuzi, kuongeza nguvu za uzalishaji, kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati, na kuwapatia wafanyakazi ujuzi wa kisasa katika zama za kidigitali.

    Amesema mawaziri hao wamepitisha mipango kadhaa muhimu, ukiwemo mfumo wa APEC wa kurahisisha biashara ya kielekitroniki ya kuvuka mipaka, mkakati endelevu wa APEC kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, na yale kuhusu kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhakikisha usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako