• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matunda yaliyopatikana katika ziara ya rais Trump nchini China yatakuwa na athari nzuri na ya muda mrefu kwa sekta ya uchumi

    (GMT+08:00) 2017-11-10 17:30:43

    Naibu waziri wa fedha wa China Bw. Zhu Guangyao leo kwenye mkutano na waandishi wa habari ameeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Donald Trump katika sekta ya uchumi wakati wa ziara ya rais Trump nchini China iliyomalizika leo. Bw. Zhu amesema makubaliano hayo yatakuwa mwongozo wa jumla na mkakati wa kuendeleza uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, na kuwa na athari nzuri ya kudumu katika miaka kadhaa ijayo.

    Naibu waziri wa fedha wa China Bw Zhu Guangyao amesema China na Marekani zimedumisha mawasiliano ya karibu katika kuratibu sera za uchumi wa jumla, zikiwemo zile za fedha na utawala, sarafu, kiwango cha kubadilishana sarafu na masuala ya mageuzi ya kimuundo ya nchi hizo na usimamizi wa uchumi wa dunia. Pande hizi mbili zitafanya juhudi za pamoja ili kuhimiza uchumi wa dunia ukue kwa nguvu, hali endelevu, uwiano na jumuishi.

    China itafuata mpango wake wa kufungua mlango na kulegeza masharti kwenye sekta ya fedha, ikiwemo kushiriki katika sekta ya benki, dhamana, na bima. Bw. Zhu anasema,

    "China itaruhusu makampuni ya nje kuwekeza na kumiliki asilimia hadi 51 ya hisa za makampuni ya hisa na dhamana nchini China, na baada ya miaka mitatu, uwekezaji wao hautakuwa na ukomo wa juu; itaondoa masharti ya kutoruhusu makampuni ya nje kumiliki asilimia zaidi ya 20 ya hisa za mabenki na mashirika ya fedha ya China, na baada ya miaka mitatu uwekezaji wao utaweza kuchukua asilimia 51 na miaka miwili baadaye, uwekezaji huo hautawekewa ukomo wa juu. "

    Bw. Zhu ameongeza kuwa China pia imetoa matakwa kadhaa kwa Marekani. Anasema,

    "China imeitaka Marekani ilegeze usimamizi wa kuuza bidhaa zake zenye teknolojia ya juu nchini China, kuyatendea kwa haki makampuni ya China yanayokwenda na kuwekeza nchini Marekani, kusaidia makampuni ya fedha ya kimataifa ya China kupata kibali cha biashara ya kifedha nchini Marekani na kuwa makini katika kutumia hatua za uokoaji wa kibiashara."

    Wakati wa ziara ya rais Trump wa China, nchi hizo mbili zimesaini makubaliano yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 250, kiasi ambacho kimeweka rekodi ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na hata rekodi ya dunia. Mtafiti wa idara ya uchumi wa kimkakati katika Kituo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Kiuchumi cha China Zhang Monan anaona kuwa China na Marekani kuangalia upya uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara, na kulenga kupanua ukubwa wa biashara ni muhimu kwa nchi hizo kujenga uhusiano wa aina mpya wa biashara kati yao.

    "Kama tunavyojua, kwa muda mrefu mikwaruzano ya kibiashara na kutokuwepo kwa uwiano wa kibiashara vimekwamisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani kupata maendeleo zaidi, lakini nchi hizi mbili zimejitahidi kutatua masuala hayo. Naona katika siku zijazo, China na Marekani zitaweza kupanua maeneo zaidi ya maendeleo na sekta zitakazofanyiwa ushirikiano wa kibiashara na kiviwanda kama vile sekta ya akili bandia, uchumi wa kidigitali, teknolojia ya biolojia na teknolojia ya hali ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako