• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watalii 266 wawasili Kenya kutoka Polanda

  (GMT+08:00) 2017-11-10 18:46:54

  Watalii 266 kutoka Poland wamewasili nchini Kenya baada ya kampuni ya ndege ya TUI Poland kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja jijini Warsaw nchini Poland hadi Mombasa.Ndege ya TUI Poland iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mwendo wa saa nne usiku ikiwa imebewba watalii 266.Rubani wa ndege hiyo Walter Wesseling amesema kampuni hiyo ilianzishga safari za moja kwa moja kutoka Warsaw hadi Mombasa kutokana na ongezeko la wasafiri.Walter amesema watalii wengi kutoka Poland wanawasili Mombasa kwa wingi kwa ajili ya kuota jua katika fuo za bahari ilhali wengine wanawasili kujionea mandhari nzuri pamoja na wanyama katika mbuga za wanyama kama vile Tsavo mashariki na magharibi.Mwenyekiti wa chama cha watalii pwani ya Kenya Victor Shitakha amesema kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kutaimarisha utalii katika maeneo ya Pwani na kote nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako