• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahudhuria mazungumzo kati ya viongozi wa jumuiya ya APEC na Umoja wa nchi za Asia ya mashariki na kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-11 17:32:02

    Rais Xi Jinping wa China jana amehudhuria mazungumzo kati ya viongozi wa jumuiya ya APEC na Umoja wa nchi za Asia ya mashariki na kusini yaliyofanyika huko Da Nang nchini Vietnam.

    Rais Xi Jinping alitoa hotuba akisema kuwa, jumuiya ya APEC ni jukwaa lenye athari kubwa kabisa la ushirikiano wa kiuchumi kwenye sehemu ya Asia na Pasifiki, Umoja wa nchi za Asia ya mashariki na kusini una nguvu na uwezo mkubwa barani Asia. Pande hizo mbili zina mawazo ya kulingana ya ushirikiano na zikitekeleza kanuni ya kufanya majadiliano ya pamoja, na kuzingatia maslahi ya pande zote, zina mustakabali mzuri ya kufanya ushirikiano.

    Habari nyingine zinasema kuwa, rais Xi Jinping wa China siku hiyo amekutana na rais Vladimir Putin wa Russia huko Da Nang. Rais Xi Jinping amesema kuwa China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na Russia ndani ya jumuiya ya APEC, kuhimiza ujenzi wa eneo la biashara huria ya Asia na Pasifiki na kupata maendeleo mapya kwa kufanya mageuzi, kuharakisha kuunda uchumi wa kufungua mlango. Rais Xi pia alimwelezea rais Putin habari kuhusu mkutano mkuu wa 19 wa CPC, na walibadilishana maoni kuhusu hali ya peninsula ya Korea na masuala mengine yanayohusu pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako