• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano usio rasmi wa 25 wa viongozi wa jumuiya ya APEC wapitisha azimio

    (GMT+08:00) 2017-11-12 17:50:47

    Mkutano usio rasmi wa 25 wa viongozi wa jumuiya ya APEC umefungwa jana huko Da Nong. Huku, Azimio lililopitishwa kwenye mkutano huo liliwataka wanachama wote waunge mkono mfumo wa biashara ya pande zote.

    Mwenyekiti wa mkutano huo Tran Dai Quang ambaye pia ni rais wa Vietnam amewaambia waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano huo, mkutano huo ulifanya majadiliano kuhusu sera na hatua za makampuni madogomadogo na ya ukubwa wa kati, maendeleo endelevu na uvumbuzi, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kupungua tishio la maafa ya kimaumbile, na kuhimiza kuwapa wanawake haki zakiuchumi.

    Azimio hilo limesema kuwa viongozi wa jumuiya ya APEC waliamua kuchukua hatua zenye nguvu kubwa zaidi na endelevu kwa pamoja, kuweka nguvu mpya kwa ushirikiano wa jumuiya ya APEC, kuhimiza ongezeko endelevu, uvumbuzi na usawa, kuzidisha umoja wa uchumi, kutafuta uwezo wa makampuni madogomadogo na ya ukubwa wa kati, kuongeza usalama wa chakula na kilimo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako