• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yakataa kuhusika na kupanga kumteka nyara kiongozi wa kidini Fetullah Gulen

    (GMT+08:00) 2017-11-13 09:00:48

    Waziri mkuu wa Uturuki Bw. Binali Yildirim amekanusha ripoti kuwa nchi hiyo inahusika na mpango wa kumteka nyara kiongozi wa kidini Fetullah Gulen aliyeko nchini Marekani. Ijumaa iliyopita jarida la Wall Street Journal liliripoti kuwa mshauri maalum wa Marekani Robert Mueller anachunguza njama inayomhusisha aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa Bw. Michael Flynn, ambaye alikutana na maofisa wa Uturuki mara mbili mwaka jana na kupewa dola milioni 15 za kimarekani ili kumteka nyara Bw. Gulen. Ubalozi wa Uturuki nchini Marekani umetoa taarifa ikiitaja ripoti hiyo kama kosa kubwa linalochekesha na lisilo na msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako