Watu 328 wamefariki baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 kwenye kipimo cha Richter kutokea kwenye eneo la mpaka kati ya Iran na Iraq jana.
Tetemeko hilo lililotokea kilomita 103 kusini mashariki mwa mji wa Sulaymaniyah, pia limesababisha watu wengine 4,000 kujeruhiwa. Zaidi ya vijiji 20 katika mkoa wa Kermanshah nchini Iran vimeathirika na huduma ya maji na umeme pia imekatika.
Nchini Iraq, watu wanane wamefariki na mamia wengine kujeruhiwa katika tetemeko hilo. Idara ya usalama katika mji wa Sulaimaniyah kaskazini mashariki mwa Iraq imesema, idadi kubwa ya vifo imetokea kwenye mkoa unaojiendesha wa Kurdistan, ambapo watu saba wamefariki na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |