• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Thamani ya makubaliano ya biashara yaliyofikiwa katika ziara ya rais wa Marekani nchini China yazidi dola bilioni 253.5

  (GMT+08:00) 2017-11-13 18:32:30

  Naibu waziri wa biashara wa China ambaye pia ni naibu mwakilishi wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Yu Jianhua leo hapa Beijing amesema, thamani ya makubaliano ya kibiashara yaliyofikiwa wakati wa ziara ya rais Donald Trump wa Marekani nchini China imefikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 253.5.

  Katika ziara hiyo, makampuni ya China na Marekani yamesaini makubaliano ya miradi 34 kwenye hafla mbili, ambayo thamani yao imefikia dola za kimarekani bilioni 253.5.

  Bw. Yu Jianhua amesema, kabla ya ziara hiyo, maofisa wa nchi hizo mbili walithibitisha miradi hiyo 34, lakini makampuni ya nchi hizo mbili pia yamesaini makubaliano mengine ya ushirikiano ambayo hayakusainiwa kwenye hafla hizo, hivyo matokeo halisi ya biashara kati ya nchi hizo mbili ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni 253.5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako