• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Serikali ina mpango wa kuanzisha vituo vya malipo kwenye barabara tano kuu

  (GMT+08:00) 2017-11-13 19:07:10

  Serikali ina mpango wa kuanzisha vituo vya malipo kwenye barabara tano kuu ambazo zitaona wa endeshaji magari wakilipa kati ya sh 120 hadi sh 3.59 kwa kila kilomita kwa miaka 30 ijayo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kitaifa ya barabara kuu Kenya Peter Mundinia amesema barabara kuu ya Nairobi-Mombasa, Nairobi-Nakuru-Mau na daraja la pili huko Nyali zitafanyiwa ukarabati na wawekezaji binafsi ambao watalipisha ada kwa wenye magari kwa kutumia barabara kuu.

  kwa barabara ambazo tayari zimekamilika kama vile barabara kuu ya Thika na Nairobi Southern Bypass, Mundinia amesema serikali hivi karibuni itatangaza zabuni kwa washirika binafsi kuanza kusimamia barabara hizo wakati wana kusanya pesa.

  Kulingana na Wizara ya Usafiri, Miundombinu, Nyumba na Maendeleo ya Mjini, akaunti ya gharama za usafiri zinajumuisha asilimia 30 ya gharama za bidhaa na huduma katika kanda zote kutokana na miundombinu mbaya na maelfu ya masaa yanayopotezwa katika trafiki kila siku .

  Magari madogo yatakuwa yanalipioshwa sh 1.20 kwa kilomita wakati pickups na vani zitalipishwa Sh1.79 kwa kilomita.

  Malori ya kati na kubwa yanalipishwa Sh2.39 na Sh3.59 kwa kilomita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako