• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aanza ziara nchini Laos

    (GMT+08:00) 2017-11-13 20:20:46

    Rais Xi Jinping wa China leo amewasili Vientiane, na kuanza ziara yake nchini Laos.

    Katika hotuba yake ya maandishi aliyoitoa kwenye uwanja wa ndege nchini humo, rais Xi amesisitiza kuwa, China na Laos ni nchi za kisoshalisti zinazoongozwa na chama cha kikomunisti, ni majirani wema, rafiki wazuri, na wenzi wema. Amesema maendeleo ya kina ya uhusiano wa kimkakati na ushirikiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili yameleta maslahi halisi kwa pande mbili na wananchi wao, pia yanatoa mchango kwa kuhimiza amani, utulivu, ustawi wa kikanda na wa dunia nzima. Amesema kuwa, anaamini kuwa kutokana na juhudi za pande hizo mbili, ziara yake hiyo itahimiza uhusiano kati ya China na Laos kuingia kiwango kipya, na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako