• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwongozo wa kwanza wa kimataifa wa matibabu yanayotumia dawa za jadi za Kichina watolewa

  (GMT+08:00) 2017-11-14 13:04:08

  Mwongozo wa kwanza wa kimataifa wa matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanayotumia dawa za jadi za Kichina umetolewa leo tarehe 14 mjini Shenzhen, kusini mwa China. Huu ni mwongozo wa kwanza wa kimataifa uliotolewa na Shirikisho la Jamii za Dawa za Kichina Duniani kuhusu matibabu yanayotumia dawa za jadi za kichina. Naibu mkurugenzi wa idara ya sera, sheria na usimamizi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Dawa za Jadi za Kichina ya China Bw. Yang Rongchen, katibu mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Dawa za Kichina Duniani Bw. Sang Binsheng, naibu meya wa mji wa Shenzhen Bw. Wu Yihuan, naibu mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa dawa za jadi za kichina ya Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) Bw. Shen Yuandong, naibu mkuu wa idara ya dawa za jadi za kichina ya Chuo Kikuu cha Hong Kong Bw. Shen Jiangang, naibu mwenyekiti wa jumuiya ya dawa za jadi za kichina ya Marekani Bw. Yang Guanhu na wataalamu wengine wa ndani na nje ya China wamehudhuria hafla ya kutolewa kwa Mwongozo huo.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, naibu mkurugenzi wa idara ya sera, sheria na usimamizi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Dawa za Jadi za Kichina ya China Bw. Yang Rongchen amesema mawasiliano ya habari ya kimataifa, shughuli za matibabu, uandaaji wa wataalamu, utafiti wa kisayansi, na usimamizi na sheria kuhusu dawa za jadi za kichina vinahitaji sana vigezo vya kimataifa. Ikiwa ina asili ya muda mrefu ya dawa za jadi, China inapaswa kufanya dawa za jadi za kichina ziwe na vigezo, pia kuwa mtungaji wa vigezo vya kimataifa vya dawa za jadi za kichina, ili iendelee kuongoza maendeleo ya dawa za jadi za kichina.

  Katibu mkuu wa Shirikisho la Jamii za Dawa za Kichina Duniani Bw. Sang Binsheng amesema tangu lianzishwe mwaka 2003, Shirikisho hilo limekuwa likihimiza kujenga vigezo vya kimataifa kwa dawa za jadi za kichina. Hadi sasa, kumekuwa na vigezo 17 kuhusu dawa za jadi za kichina katika Shirika la Viwango la Kimataifa ISO, lakini bado hakuna mwongozo wa kimataifa wa matibabu yanayotumia dawa za jadi za kichina. Ameeleza kuwa madhumuni ya mwanzo ya Shirikisho la Jamii za Dawa za Kichina Duniani kutunga Mwongozo huo ni kutafuta mtindo mpya katika kutunga mwongozo wa matibabu yanayotumia dawa za jadi za kichina duniani. Shirikisho hilo litatunga kanuni kwa kufuata vigezo vya kimataifa vya ISO na kusoma mwongozo wa matibabu yenye msingi wa ushahidi wa Shirika la Afya Duniani WHO, na kutafuta na kukamilisha utaratibu wa utungaji wa mwongozo wa kutibu wagonjwa kwa kutumia dawa za jadi za kichina wa Shirikisho la Jumuiya za Dawa za Kichina Duniani. Ameeleza matumaini yake kuwa baada ya Mwongozo huo kutolewa, utaweza kuenezwa katika maeneo mengi duniani.

  Mtungaji mwandamizi wa Mwongozo huo ambaye ni mtafiti wa Taasisi ya Sayansi za Dawa za Kichina ya China Profesa Tong Xiaolin amesema ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaofuatiliwa sana kote duniani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusababisha vifo na ulemavu. Lakini dawa za jadi za kichina zina uwezo mkubwa katika kujikinga na ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha mwanzo, kudhibiti hali ya kukosa utaratibu wa kawaida wa umetaboli kutokana na ugonjwa wa kisukari na kutibu magonjwa mengine yanayosababishwa na ugonjwa huo. Mwongozo huo ni mkusanyiko wa mafanikio ya utafiti wa matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanayotumia dawa za kichina ya ndani na nje ya China katika nusu karne iliyopita, na inatarajiwa kuwa Mwongozo huo utaweza kutoa mchango kwa shughuli za kutibu wagonjwa za madaktari wa matibabu ya kichina wa ndani na nje ya China, utungaji wa sheria na utaratibu wa kimataifa wa dawa za jadi za kichina, ujenzi wa vigezo vya kimataifa vya dawa za jadi za kichina, na mpango wa maendeleo ya dawa za jadi za kichina kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutoa mfano wa kuigwa duniani kwa matibabu ya magonjwa makubwayanayotumia dawa za jadi za kichina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako