• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Laos wakutana Vientiane

  (GMT+08:00) 2017-11-14 14:11:14

  Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Laos Bw. Bounnhang Vorachit, wamekutana mjini Vientiane, na kukubaliana nchi zao kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja yenye umuhimu wa kimkakati.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa China kufanya ziara nchini Laos katika miaka 11 iliyopita. Wakati wa mazungumzo yao, pande hizo mbili zimezungumzia mafanikio yaliyoyapatikana kwenye uhusiano wa nchi zao, na kukubaliana kuimarisha mawasiliano na kufundishana, kusukuma mbele hatua za mageuzi na ufunguaji mlango za China, na mchakato wa mageuzi ya Laos.

  Nchi hizo mbili pia zitaendelea kuimarisha urafiki wa jadi kati yao, na kujitahidi kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati hadi katika ngazi mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako