• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Afrika kufanyika nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2017-11-14 18:02:13

  Maonesho ya mwaka 2017 ya ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Afrika yatafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 16 Desemba huko Nairobi, Kenya. Maonesho hayo yanayohusishaa teknolojia za upashanaji habari, kilimo, utengenezaji wa vyakula, miundombinu, ujenzi wa majengo, mitambo ya mashine na sekta nyinginezo, ni maonesho makubwa zaidi yanayoandaliwa na Shirika la Kuhimiza Biashara la China barani Afrika, na madhumuni yake ni kujenga jukwaa jipya la kuhimiza uwekezaji na biashara kati ya China na Afrika.

  Afrika ni sehemu muhimu katika pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", pia ni lengo muhimu la kuwekezwa la kampuni za China. Takwimu zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilikuwa dola za Kimarekani bilioni 85.3, na kuongezeka kwa asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Wakati huo huo thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa kampuni za China barani Afrika ilikuwa dola za kimarekani bilioni 1.6, na kuongezeka kwa asilimia 12.

  Naibu mkuu wa Shirika la Kuhimiza Biashara la China Bw. Chen Zhou amesema, ukubwa wa eneo la maonesho hayo utakuwa mita za mraba zaidi ya 2,300.

  "Kampuni 56 kutoka mikoa 18 ya China zikiwemo kampuni kuu ya mtandao wa umeme ya China, kampuni ya ujenzi wa mawasiliano ya barabarani ya China, na kampuni ya umeme wa nyuklia ya China zitashiriki kwenye maonesho hayo, na kuonesha bidhaa zenye sifa nzuri na teknolojia za hali ya juu za ujenzi wa reli, barabara, miundombinu, upashanaji habari, mitambo ya mashine, uzalishaji, utengenezaji wa mazao ya kilimo na nyinginezo."

  Balozi wa Kenya nchini China Bw. Michael Kinyanjui anaona maonesho hayo yatajenga daraja la ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Afrika, na kuweka jukwaa lenye ufanisi kwa ajili ya kuhimiza zaidi biashara kati ya pande hizo mbili.

  "Maonesho hayo yatazipatia kampuni kubwa na za ukubwa wa kati za China jukwaa la kutafuta fursa mpya barani Afrika, na kupanua soko kwa kushirikiana na kampuni za Kenya na nchi nyingine za Afrika. Wakati huo huo, maonesho hayo pia yatawapa washiriki wa Afrika nafasi ya kuwasiliana na kampuni za China ili kujenga uhusiano wa kiwenzi, na jukwaa la kuongeza mauzo yao nchini China. Maonesho hayo yatahimiza uwekezaji na biashara kati ya Afrika na China."

  Hivi sasa ushirikiano kati ya China na Afrika unafanyika kwa kina, upana na kwa hamasa kubwa. Kenya ni nchi ya mwanzo kufanya ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Afrika. Naibu mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya China na Afrika Bw. Zhou Chao amekadiria kuwa, ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Kenya utaendelea kwa kasi, ambapo uwekezaji wa China kwenye mtandao wa reli na barabara za kasi, safari za ndege na viwanda nchini Kenya utaongezeka kwa haraka sana. Na hali hii pia itakuwa mfano mzuri kwa nchi jirani na Kenya.

  "Ikiwa mwanzilishi na mwanachama muhimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, moja ya makao makuu ya ofisi za Umoja wa Mataifa, Kenya ni kitovu cha mambo ya uchumi na fedha cha ukanda wa Afrika Mashariki. Shughuli za kampuni za China nchi Kenya zitakuwa mfano kwa nchi jirani na Kenya zikiwemo Tanzania, Ethiopia, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan, na hata Afrika nzima. Kwa kampuni za China zinazopanga kufanya shughuli zake barani Afrika kwa muda mrefu, maonesho hayo yatakuwa fursa nzuri ya kujitangaza, kuchunguza mazingira ya kibiashara, na kuwasiliana na kampuni za Afrika."

  Wakati wa maonesho hayo, baraza la ushirikiano wa uzalishaji kati ya China na Afrika, mkutano wa kutangaza teknolojia na bidhaa, mkutano wa mawasiliano ya miradi kati ya kampuni, na mkutano wa kuhimiza uwekezaji kwenye nchi nne za Afrika pia itafanyika. Hivi sasa maandalizi ya maonesho hayo yanaendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako