• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania tazuia mifugo 10, 000 wa Rwanda na Uganda

  (GMT+08:00) 2017-11-14 19:07:12

  Serikali nchini Tanzania imezuilia zaidi ya mifugo 10,000 kutoka nchi jirani za Uganda na Rwanda.

  Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina amesema mifugo hao watauzwa kwenye mnada kama walivyofanyiwa wale waliokamatwa wakitokea nchini Kenya.

  Waziri Mpina akijibu swali bungeni alilaumu wafugaji wa Rwanda na Uganda kwa kukiuka sheria za Tanzania na kuvukisha mifugo wao mpakani.

  Hivi karibuni serikali ya Tanzania iliwauza kwa mnada zaidi ya ng'ombe 1,300 waliokuwa wameingia nchini humo kwa malisho kutoka Kenya.

  Rais wa Tanzania John Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa serikali haitakubali mifugo wowote kuingia nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako