• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China asisitiza kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya uchumi wa nchi za Asia mashariki

  (GMT+08:00) 2017-11-14 19:09:21

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo asubuhi amehudhuria mkutano wa 20 kati ya viongozi wa Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki na China, Japan na Korea Kusini kwenye kituo cha mkutano cha kimataifa nchini Philippines.

  Katika mkutano huo, Bw. Li Keqiang amesema, katika miaka 20 iliyopita mfumo wa ushirikiano kati ya Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki na China, Japan na Korea Kusini umeendelea kuboreshwa, na sekta za ushirikiano zimeongezeka hatua kwa hatua, ambao ni mfumo kamili na uliopata mafanikio zaidi kwenye eneo la Asia. Amesema mfumo huo umetoa mchango mkubwa kwa kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa eneo la Asia ya mashariki.

  Bw. Li amesema, China inatarajia mkutano huo utaendelea kukusanya maoni ya pamoja, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono utandawazi wa eneo hilo, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya uchumi wa Asia mashariki, kuwanufaisha watu wa nchi hizo, na pia kuongeza nguvu kwa uchumi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako