• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi ya China yamrudisha mhalifu wa Marekani

    (GMT+08:00) 2017-11-14 19:24:56

    Polisi ya China leo imemrudisha mtu mmoja anayetuhumiwa kwa uhalifu aliyekimbilia China kutoka Marekani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pudong, Shanghai.

    Hatua hiyo imetokana na ombi la idara ya sheria ya Marekani. Wawakilishi wa polisi ya China na ubalozi mdogo wa Marekani mjini Shanghai wamethibitisha na kushuhudia mchakato wa kurudishwa kwa mhalifu huyo, ambaye ni wa nne kurudishwa Marekani na polisi ya China kwa mwaka huu, huku Marekani nayo ikiwarudisha wahalifu wawili nchini China.

    Wizara ya usalama wa umma ya China imesema, wakati wa ziara ya rais Donald Trump wa Marekani nchini China, marais wa nchi hizo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na usalama wa mtandao wa Internet. Pia wamesisitiza kuwa, kila upande hautakuwa sehemu ya kuepuka adhabu kwa wahalifu wa upande mwingine, na kuchunguza mfumo wa ushirikiano wenye ufanisi wa muda mrefu katika kukamata wahalifu wanaotoroka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako