• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tour Du Rwanda, Simon Pellaud mshindi hatua ya pili

    (GMT+08:00) 2017-11-15 10:13:53
    Simon Pelluad wa Uswisi amefanikiwa kushinda hatua ya pili yam bio za kimataifa za Rwanda ambapo kwa kutumia saa 4 na dakika 32 alimaliza kilomita 180 ambazo ni umbali kati ya mji wa Nyanza na Rubavu.

    Nafasi ya pili katika hatua hiyo ilitwaliwa na Matthieu Jeannes wa Ufaransa na Didier Munyaneza akikamata nafasi ya tatu lakini bingwa mtetezi wa Mbio hizo Valens Ndayisenga akishindwa kutamba baada ya jana kuambulia nafasi ya saba.

    Mbio hizo zinaendelea kwa hatua ya tatu, yenye umbali wa kilomita 95 kuanzia Rubavu hadi mjini Musanze.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako