• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Milipuko imesikika mjini Harare muda mfupi baada ya mkuu wa majeshi kukosolewa

    (GMT+08:00) 2017-11-15 11:27:32

    Milipuko mikubwa kadhaa imesikia mjini Harare mapema leo, baada ya jeshi kutishia kuingilia kati kuondoa mivutano ya kisasa kuhusu nani atakuwa mrithi wa Rais Robert Mugabe.

    Wanajeshi wamesambaa mjini Harare na kutwaa udhibiti wa shirika la utangazaji, baada ya chama cha Zanu-PF kumshutumu mkuu wa majeshi wa Zimbabwe Constantino Chiwenga kwa kauli ya kihaini.

    Msemaji wa chama Bw Simon Moyo amesema kauli ya Bw Chiwenga ni kitendo cha kihaini kinachoweza kuvuruga amani na utulivu wa taifa. Amesema taarifa iliyotolewa na Bw. Constantino Chinwenga haiwakilishi maoni ya viongozi wengine wa jeshi, na ni kitendo chake binafsi kinachokusudia kuchochea mgogoro na kuharibu utaratibu wa kikatiba.

    Jumatatu wiki hii Bw Chinwenga alitoa taarifa kwa chama cha ZANU-PF kukitaka kusimamisha kuwafukuza wanachama waliowahi kushiriki kwenye mapambano ya ukombozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako