• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetemeko la ardhi lasababisha hasara za dola za Marekani milioni 450 nchini Iran

    (GMT+08:00) 2017-11-15 17:59:38

    Idara inayosimamia serikali za mitaa nchini Iran imesema, thamani ya hasara iliyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni nchini humo imefikia dola za Marekani milioni 450.

    Kwa mujibu wa ripoti ya jimbo la Kermanshah, nyumba elfu 11 zilibomoka, na kwamba hasara itaendelea kuongezeka kuendana na uharibifu wa barabara na miundombinu.

    Habari zinasema, rais Hassan Rouhani wa Iran amehimiza idara husika kuongeza nguvu za uokoaji, na kuahidi kuwa serikali itatenga kiasi cha fedha kusaidia waathirika kujenga nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako