Baraza hilo lenye nchi wajumbe 15 lilipitisha Azimio namba 2385 la kuongeza muda huo kwa nchi za Somalia na Eritrea, ambapo nchi 11 zilipiga kura ya ndio huku Bolivia, China, Misri na Russia zikiacha kupiga kura hiyo. Baraza hilo pia limeongeza muda wa kikosi cha usimamizi katika nchi za Somalia na Eritrea mpaka mwisho wa mwaka ujao, na kutambua kuwa wakati wa majukumu yake ya sasa na yaliyopita, kikosi hicho kimeshindwa kupata ushahidi kamili kuwa Eritrea inaunga mkono kundi la Al Shabaab la Somalia.
Akizungumzia hatua hiyo, naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, China haikupiga kura hiyo kwa sababu inaona kuwa azimio hilo linahitaji kufanyiwa maboresho kwani kuondoa vikwazo ni njia ya kusaidia kutatua masuala husika ya kikanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |