• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la BASIC lasisitiza kuharakisha utekelezaji wa ahadi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:13:21

    Mawaziri wa nchi nne zinazounda kundi la BASIC wanaohudhuria mkutano wa hali ya hewa wa Bonn wametoa taarifa ya pamoja wakisisitiza kuharakisha utekelezaji wa ahadi na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya mwaka 2020.

    Mkutano wa 25 wa mawaziri nchi hizo zikiwemo Brazil, China, Afrika Kusini na India ulifanyika hivi karibuni huko Bonn, Ujerumani, ambapo nchi hizo zilisisitiza kuwa inapaswa kuweka ajenda maalum ya kutatua masuala husika. Mkutano huo pia ulitarajiwa kupitisha mswada utakaojadiliwa mwaka kesho ambao utaonesha maombi ya pande mbalimbali na sehemu mbalimbali za makubaliano ya Paris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako