• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Kampuni ya China yasaini ushirikiano Shs11m kwa ajili ya ufadhili wa masomo

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:36:08

    Wanafunzi werevu ambao hawana uwezo wa kifedha katika chuo cha Luyanzi,wilaya ya Bweyogerere nchini Uganda wana kila sababu ya kutabasamu baada ya chuo hicho na kampuni ya ujenzi ya China ya Henan Guoji Group kusaini ushirikiano wa Sh10.8m kwa ajili ya kufadhili masomo ya wanafunzi wanne maskini katika chuo hicho kila mwaka.

    Akizungumza wakati wa utoaji wa ufadhili chuoni humo jana,Kamishna wa wizara ya elimu Uganda,Ismael Mulindwa alipongeza msaada huo na kuwashukuru wachina kwa kuikuza lugha ya kichina.

    Alisema ufadhili huo wa masomo unaimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa pande mbili kati ya Uganda na China.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mirembe Villas,mojawapo ya wachangiaji wa mpango wa ufadhili wa masomo,Bi Shen Jie, alisema elimu kwa watoto maskini ni muhimu.

    Alisema kuna wachina wengi walio na moyo wa kuwasaidia watoto wanaotoka familia maskini haswa katika sekta ya elimu.

    Alisema wanaamini kuwa kupitia elimu,wanafunzi wanaweza kuendeleza nchi ya Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako