• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika watoa wito kwa Zimbabwe kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia ya kisheria

    (GMT+08:00) 2017-11-16 10:22:21

    Umoja wa Afrika umeitaka serikali ya Zimbabwe na jeshi la nchi hiyo kutatua mgogoro wa kisiasa kwa kufuata katiba ya nchi hiyo.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amezihimiza pande zote kuheshimu katiba ya Zimbabwe na vifungu husika vya katiba ya Umoja wa Afrika. Amesema umoja huo unafuatilia hali ya nchini Zimbabwe, na kuahidi kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, ili kuhakikisha mgogoro wa kisiasa nchini humo unatatuliwa kwa njia ya amani.

    Mapema siku hiyo, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa SADC, alitoa taarifa akieleza ufuatiliaji wake kuhusu hali ya kisiasa nchini Zimbabwe, na kuzitaka pande zote zijizuie na kuondoa mvutano wa kisiasa nchini humo kwa njia ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako