• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za kiarabu zahimiza ufumbuzi wa mgogoro wa Libya

    (GMT+08:00) 2017-11-16 10:23:03

    Mawaziri wakuu wa Misri, Tunisia na Algeria Jumatano wamehimiza pande zinazopambana nchini Libya kufikia mwafaka kuhusu ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini humo.

    Kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Cairo, waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Sameh Shoukry amesisitiza kuwa nchi hizo tatu zimekuwa zikichukua hatua kwa pamoja, ili kutimiza utulivu nchini Libya na kuzuia nchi za nje zisiingilie kati mambo ya ndani ya Libya .

    Mawaziri hao wamekumbusha juhudi zilizofanywa na nchi zao katika miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya kufanikisha makubaliano kati ya pande zinazopambana nchini Libya.

    Pia wanafurahia juhudi za mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, na kueleza uungaji mkono kwa mpango wake wa kutatua mgogoro wa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako