• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Libya atarajia balozi za nchi mbalimbali zitafungua tena ofisi zao mjini Tripoli

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:27:58
    Waziri wa mambo ya nje wa Libya Bw. Mohamed Sayala amesema anatarajia balozi za nchi mbalimbali nchini Libya zitafungua tena ofisi zao mjini Tripoli.

    Bw. Sayala amesema, wizara ya mambo ya nje ya Libya imefanya maandalizi na kutoa huduma ya ulinzi, kusaidia ofisi hizo za ubalozi kuanza tena kutoa huduma ili kuwawezesha walibya kupata visa na kuongeza mawasiliano kati ya Libya na nchi mbalimbali.

    Bw. Sayala pia amesema, hivi sasa, Italia, na Uturuki zimeanza kutoa huduma ya visa kupitia balozi zao mjini Tripoli, na kwamba wizara yake inazungumza na Marekani kuhusu masharti ya kufungua tena ofisi za ubalozi wake nchini Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako